Ni vita nyengine kati ya Chelsea dhidi ya Everton mara baada ya klabu hizo kucheza uwanjani na Chelsea kuendeleza ubabe wake, sasa ni vita ya sokoni kati ya klabu hizo.
Chelsea imekuwa inamfukuzia nyota muhispania anayeichezea Swansea, Fernando Llorente lakini sasa Everton na wao wanataka kuitibulia Chelsea juu ya nyota huyo aliyewai kuwa chini ya kocha Antonio Conte wa Chelsea ambaye kipindi hicho walikuwa wote Juventus.
Conte anamfukuzia Llorente kwa karibu toka dirisha dogo la usajili mwezi wa kwanza ambapo Swansea iligoma kumuuza ikiwa kwenye kampeni za kujitetea kutokushuka daraja, lakini sasa Conte amekuwa akimtazamia nyota huyo katika kukiimarisha kikosi chake.
No comments:
Post a Comment