Tuesday 11 July 2017

Chelsea kuelekea msimu mpya wa 2017-2018

Chelsea, klabu inayopatikana magharibi mwa jiji la London, jiji kubwa ambalo linatajwa kuwa mashuhuri zaidi nchini Uingereza. Klabu ambayo inashikilia ubingwa wa Ligi Kuu nchini hapo ambao imeutwaa kwa kishindo msimu uliopita katika uongozi wa meneja mpya, Antonio Conte ambaye amekuwa muitalia wa 5 kutwaa taji hilo.

Klabu hiyo imekuwa na maandalizi mbalimbali kuelekea msimu mpya wa 2017-2018, msimu huu wakiwa wanashiriki kucheza klabu bingwa ya Ulaya maarufu kama Uefa Champions League imekuwa na jitihada kubwa za kujiandaa na msimu huo ambao unaonekana kuwa mgumu kwa klabu hiyo.

Usajili klabuni hapo
Mpaka sasa klabu hiyo imeshawasajili wachezaji wawili ambao wanaingia kwenye kikosi cha wakubwa ambao ni Willy Caballero aliyeachwa na Man city na Antonio Rudiger aliyetokea As Roma. Wachezaji hao ambao wamekuja kama kuziba mapengo ambapo Rudiger ameziba pengo la gwiji John Terry aliyejiunga na Aston Villa wakati kwa Caballero ni kama amekuwa mrithi wa kipa namba mbili wa klabu hiyo aliyeuzwa kwenda Bournemouth, Asmir Begovic kwa dau la paundi milioni 10.

Ingawa bado kuna wengine wanatajwa kuwaniwa kwa karibu na klabu hiyo.

Mpaka sasa walioondoka klabuni hapo ni Cuadrado aliyesajiliwa na Juventus, Nathan Ake naye alijiunga na Bournemouth, Betrand Traore aliyetimkia Olympique Lyon wakati na Loftus-Cheek nae akitajwa kuungana na Crystal Palace kwa mkopo, hao ni baadhi tu. Idadi ambayo haifanani na waliosajiliwa na klabu hiyo.

Michezo ya kirafiki
Michezo hii ina faida kwa klabu ambapo wachezaji hujiweka sawa mara baada ya mapumziko ya msimu ulioisha.

Chelsea itacheza michezo hii ya kirafiki katika bara la Asia ambapo itacheza na Arsenal siku ya tarehe 22 ya mwezi July alafu itapumzika kwa siku kadhaa kabla ya kumenyana na Bayern Munchen siku ya tarehe 25 mwezi July na kumalizia na Inter Milan siku ya tarehe 28 mwezi July.

Lakini pia Chelsea inategemea kucheza michezo katika uwanja wake wa Cobham ambapo mashabiki hawatoweza kuingia.

No comments:

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://www.facebook.com/photo.php?fbid=1405295759685033&set=t.100007345536843&type=3&theater} The moment you come is the moment we let you go away {facebook#https://www.facebook.com/jeshilangu}
Powered by Blogger.