Klabu ya Everton imepangua dau la Chelsea ililoliweka juu ya kumsajili nyota wake raia wa Uingereza, Ross Barkley. Chelsea ilipeleka dau la paundi milioni 25 ili kumsajili nyota huyo ambaye alishadai kuondoka klabuni hapo kusaka changamoto nyengine nje ya klabu hiyo.
Chelsea imekuwa ikimtaka kiungo huyo ili kujiimarisha na wachezaji katika kipindi hiki ambacho klabu hiyo inashindana katika michuano mingi ikiwamo ya klabu bingwa Ulaya.
No comments:
Post a Comment