Wednesday 30 August 2017

Ni Drinkwater na Kante tena

Danny Drinkwater bado anaendelea kuwatoa udenda Chelsea na mashabiki wote wa Chelsea dunia nzima. Huenda muda wowote nyota huyo mwenye miaka 27 akaungana na nyota wa Chelsea, N'golo Kante ambaye kabla walishacheza wote timu moja wakiwa Leicester city kabla ya Kante kuamia Chelsea.

Drinkwater analazimisha kuondoka Leicester akitaka ajiunge Chelsea, mpango ambao Leicester wanautilia ngumu mara baada ya kukataa ofa ya Chelsea ambayo ipo tayari kutoa paundi milioni 27 ingawa wao Leicester wanataka kiasi cha paundi milioni 30.

Chelsea ina upungufu wa wachezaji raia wa Uingereza ambapo kwenye kikosi cha kwanza kuna raia wa Uingereza mmoja tu ambaye ni Gary Cahill ambaye pia anaweza akapoteza nafasi katika kikosi cha kwanza muda wowote, na kisheria za nchi ya Uingereza ambapo timu hiyo inapatikana inakataza klabu kutokuwa na mchezaji hata mmoja wa nchini humo kwa maana hiyo Chelsea inasaka wachezaji wa kiingereza ambapo mpaka sasa inatajwa kuwafukuzia nyota kama Ross Barkley, Oxlade Chamberlain, Jamie Vardy na Danny Drinkwater.

Chelsea kukamilisha usajili wa Llorente leo jumatano

Imesalia siku moja tu kabla dirisha la usajili halijafungwa. Ambapo linatarajiwa kufungwa usiku wa tarehe 31-Agosti mishale ya saa 5:59 usiku.

Na Chelsea inataka kutimiza jitihada za kumsajili nyota wa Swansea, Fernando Llorente ambapo Chelsea ipo tayari kutoa kisi cha paundi milioni 12 ingawa Swansea wanatazamia kumuuza mshambuliaji huyo kwa dau la kuanzia paundi milioni 15.

Lakini pia kuna kikwazo kingine juu ya usajili wa mchezaji huyo ambapo inaelezwa Swansea itakuwa tayari kumuuza nyota huyo endapo klabu yenyewe itafanikiwa kukamilisha usajili wa Wilfred Bony kutoka Manchester city.

Chelsea yaifata tena Bayern

Chelsea imeifata tena klabu mabingwa wa Bundesliga, bayern munich mara baada ya mara ya kwanza kuifata klabu hiyo juu ya kumtaka nyota wa klabu hiyo Renato Sanchez sasa klabu hiyo imepeleka dau kwa klabu hiyo kumsajili nyota mwengine wa klabu hiyo, Rafinha.

Rafinha mwenye miaka 31 anatakiwa na Chelsea mara baaada ya klabu hiyo kuikosa saini ya nyota mwingereza, Alex Oxlade Chamberlain na sasa Conte anamtazama mlinzi huyo kuwa mbadala wa Chamberlain katika jitihada zake za kukiimarisha kikosi.

Rafinha aliyejiunga na Bayern mwaka 2011 anaonekana kuwa na nafasi finyu mbele ya mlinzi Joshua Kimmich anayetumika sana na Bayern kuliko mlinzi huyo.

Costa huenda akaondoka muda wowote

Mshambuliaji wa Chelsea, Diego Costa ambaye ni raia wa Hispania huenda akajiunga na klabu moja nchini Hispania ili aichezee kes mkopo kabla ya kujiunga na klabu anayoitaka ya Atletico Madrid.

Habari zilizopo ni kwamba huenda Diego Costa akakubali kujiunga na klabu ya Las Palmas inayooshiriki ligi moja na klabu ya Atletico Madrid ili aichezee klabu hiyo mpaka pale Atletico itakapotoka kifungoni ambapo klabu hiyo imefungiwa kutokusajili mpaka ukifika mwezi wa Januari.

Diego Costa alipokea ujumbe kutoka kwa kocha wa Chelsea, Antonio Conte kwamba aondoke kwenye klabu hiyo kwa kuwa hayupo kwenye mipango ya timu. Lakini pia ikumbukwe kwamba Diego Costa hajaitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Hispania kwa vile mpaka sasa hajachheza mchezo wowote wa kiushindani.

Usajili umekamilika; Gibbs ajiunga na West Brom

Klabu inayoshiriki ligi kuu Uingereza maarufu kama Premier League, West Bromwich Albion imefanikisha dili la kumsajili nyota kutoka Arsenal, Kierran Gibbs.

Gibbs amejiunga na klabu hiyo kutokana na ufinyu wa namba katika kikosi cha Arsene Wenger na amejiunga na klabu hiyo iliyokuwa inamfukuzia kwa muda sasa ambapo pia klabu ya Watford nayo ilionyesha nia ya kumsajili mlinzi huyo.

Mashabiki; Cahill sababu ya Chamberlain kuikataa Chelsea

Kulikuwa na kunaendelea kuwepo habari na tetesi juu ya Chelsea kumsajili winga wa Arsenal ambaye ni raia wa Uingereza, Oxlade Chamberlain. Na katika usajili huo ambao kwa sasa unaonekana kuvunjika mara baada ya Chamberlain kuona nafasi ambayo atakuja kucheza akiwa Chelsea ni winga beki na yeye anapendelea kucheza kama kiungo au mchezaji wa kati, na si unajua kama nahodha wa Chelsea Gary Cahill ndiye alikuwa anatumika kumshawishi nyota huyo ili atue klabuni hapo. Sasa mashabiki wameanza kuleta utani kwamba sababu ya Chamberlain amegoma kuja Chelsea kisa ni Gary Cahill.

Gary Cahill alimwambia Chamberlain kwamba kuja kwake Chelsea kutamfanya kushinda mataji mengi kma ilivyokuwa kwake ambaye naye alisajiliwa na Chelsea akitokea klabu ya Bolton na mpaka sasa amehusika katika mataji mengi ambayo Chelsea imeshinda, kwa maana hiyo kama Chamberlain naye akija Chelsea basi atashinda mataji mengi kauli ambayo imetafsiriwa kivingine na mashabiki wengi wa soka kwamba kuja kwa Chamberlain basi atatumika kama mlinzi kama ilivyotokea kwa Cahill ambaye naye ni raia wa Uingereza.

Johnny MaLcom x

{picture#https://www.facebook.com/photo.php?fbid=1405295759685033&set=t.100007345536843&type=3&theater} The moment you come is the moment we let you go away {facebook#https://www.facebook.com/jeshilangu}
Powered by Blogger.