Nyota na winga wa Chelsea, Jeremie Boga huenda akaondoka Chelsea na kujiunga kwa mkopo na klabu ya Birmingham inayoshiriki ligi daraja la kwanza la nchini Uingereza maarufu kama Championships.
Boga aliyefanya vizuri na kujulikana katika mchezo dhidi ya Arsenal barani Asia ambapo Chelsea ilikuwa dhiarani kujiandaa na msimu mpya. Boga aliingia kuchukua nafasi ya Pedro Rodriguez ambaye alitolewa kwa majeruhi.
Endapo Boga akijiunga na klabu hiyo kwa mkopo atakuwa nyota wa 28 kuondoka kwa mkopo katika dirisha hili. Wengine ni kama Lewis Baker, Kurt Zouma, Loftus Cheek, Piazon na wengine kibao.
No comments:
Post a Comment