Friday 3 March 2017

Mjue zaidi Eden Hazard

Jina kamili; Eden Michael Hazard
Tarehe ya kuzaliwa; 7-January-1991
Mahali alipozaliwa; La Louviere, Ubelgiji
Urefu; Meta 1.73 (futi 5 na inchi 8)
Timu anayochezea kwa sasa; Chelsea
Jezi namba; 10
Utaifa; Ubelgiji

Eden Hazard ambaye alizaliwa katika familia ya wacheza mpira baba yake Thierry ambaye alicheza soka kwa nafasi ya mlinzi na huku mama yake Carie akiwa kama mshambuliaji alianza soka lake akiwa na miaka 4 mwaka 1995 katika klabu ya mtaani ya Royal Stade Brainois ya Ubelgiji ambapo alicheza hapo mpaka mwaka 2003 wakati huo akiwa na miaka 12 kabla ya kwenda tena katika timu ya mtaani au academy ya Tubize ambayo aliichezea mpaka mwaka 2005.

Ilipofika mwaka 2005 wakati huo wazazi wake wakiwa tayari washaachana na kucheza soka walikuwa tayari wanajihusisha na mchezo huo tu kama makocha na waalimu wa mchezo huo ndipo Eden Hazard akapatiwa taarifa kwamba academy au shule ya mchezo wa soka ya Lille ya Ufaransa ilipendezwa na soka lake na inabidi asafiri kwenda kucheza soka nchi tofauti na aliyozaliwa na kukulia.

Alikubali kwenda huko haswa akipata support kubwa kutoka kwa wazazi wake wakimpa moyo kwa kuwa na wao walikiamini kipaji chake na waliona ni nafasi kwake kuweza kung'aa ukizingatia akifika kule atapata nafasi kubwa ya kukomaa kwa kuwa kuna vifaa vingi vya kufanya mazoezi tofauti na Tubize ambayo ilikuwa ni klabu tu ya mtaani.

Alipofika Lille alicheza kwa mafanikio makubwa na ndipo timu ikampandisha kutoka academy mpaka kwenye kikosi cha wakubwa hiyo ikiwa mwaka 2007. Na November mwaka huo akawa chini ya kocha, Rud Garcia na katika msimu huo akacheza mechi zote na kuonekana kuwa na kipaji cha pekee na kuchaguliwa kuwa mchezaji bora chipukizi na chama cha National Union of Professional Footballers (UNFP) na kuwa mchezaji wa kwanza chipukizi kushinda kutoka nje ya Ufaransa kushinda tunzo hiyo.
Msimu wa 2009-2010 pia alishinda pia tunzo hiyo na kuwa mchezaji wa kwanza kushinda tunzo hiyo mara mbili.

Lakini pia msimu huo huo UNFP wakamchagua kuwa mchezaji bora wa msimu na kuwa mchezaji mdogo zaidi kushinda tunzo hiyo. Lakini pia alipewa tunzo na jarida la Guerin Sportivo katika tunzo za Bravo Awards kama mchezaji bora wa msimu wa 2010-2011 kwa kiwango alichokionyesha katika kuisaidia timu yake kutwaa makombe mawili ndani ya msimu mmoja yaani kombe la ligi kuu Ufaransa na kombe la Coupe de France msimu huohuo.

Mnamo tarehe 04-June-2012 muda kidogo kupita baada ya Chelsea kutwaa kombe la klabu bingwa ya Ulaya (Uefa Champions league) ndipo Eden Hazard alitangaza kujiunga na Chelsea na kupitia mtandao wa Twitter alitweet kwa kuandika "I'm signing for the Champions League winner" akimaanisha "nimesaini na mashindi wa klabu bingwa" na alisajiliwa kwa dau la £32milioni (paundi milioni 32). Ambapo pia inasadikika usajili huo ulichochewa na Didier Drogba aliyempigia simu Gervinho ambaye anatoka taifa moja na Drogba lakini kwa muda huo alikuwa akiichezea Lille yaani akiwa timu moja na Hazard. Ndipo Drogba aliyekuwa karibu alimpigia simu Gervinho na kutaka kumpa simu Hazard ili waongee na ndipo Drogba akampatia simu Abramovic ambaye alikuwa pembeni na ndipo Abramovic akatumia nafasi hiyo kuweza kumshawishi Hazard.

Baada ya kutua Chelsea alikabidhiwa jezi yenye namba 17 ambayo mwanzo ilikuwa inavaliwa na Jose Bosingwa na mchezo wake wa kwanza wa kimashindano ulikuwa dhidi ya Manchester city katika mchezo wa ngao ya hisani na kushuhudia Chelsea ikifungwa 3-2, na wiki moja baadae akaiongoza timu yake katika mchezo wa ligi kuu na kufanikiwa kutoa pasi ya mwisho na Ivanovic kufunga goli na akasababisha penati ambayo ilipigwa na Lampard na mchezo huo kuisha kwa Chelsea kumfunga Wigan 2-0.

March-2013 mchezaji nyota wa Chelsea ambaye kwa sasa amestaafu soka, Frank Lampard alisema "I've said to him, he has the world at his feet and with the way he is playing and the ability he has on the ball is scaring the life of people" akimaanisha "nimemwambia, kwenye miguu yake kuna dunia na kwa jinsi anavyocheza na uwezo alionao anaogopesha maisha ya watu"

Ambapo pia gwiji wa soka Zinedine Zidane aliwai kusema neno juu ya mchezaji huyo, alisema "Eden ni mchezaji mzuri sana anayetumia akili na uwezo mkubwa sana. Atakuwa ni nyota sana baadae"

Si hao tu ila magwiji kibao washatoa neno juu yake, watu kama Jose Mourinho na hata Thierry Henry.

Eden Hazard pia ni mme wa mke mmoja aitwaye Natacha van Honacker ambao wamejaaliwa kupata watoto watatu wote wakiume. Wa kwanza anaitwa Yannis aliyezaliwa September-2010, wa pili anaitwa Leo aliyezaliwa February-2013 na wa tatu anaitwa Samy aliyezaliwa September-2015.

Eden Hazard ni mtoto wa kwanza katika familia ya wenye watoto wanne ambapo anayemfata ndiye anaitwa Thorgan Hazard ambaye alishawai kusajiliwa na Chelsea kabla ya kuuzwa kwenda Borrusia Monchenglbach ya Ujerumani.

Jambo ambalo labda hujawai kulijua ni kwamba Eden Hazard alicheza mpira toka akiwa tumboni kwa mama yake. Kivipi? Mama yake ambaye alikuwa naye ni mcheza soka hakujigundua kama ana ujauzito mpaka alipopima na kugundulika ana ujauzito wa miezi mitatu kwa maana hiyo muda wote huo alikuwa anaendelea kucheza mpira kwa miezi mitatu ndipo alipogundulika ana ujauzito na akaachana na soka.

No comments:

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://www.facebook.com/photo.php?fbid=1405295759685033&set=t.100007345536843&type=3&theater} The moment you come is the moment we let you go away {facebook#https://www.facebook.com/jeshilangu}
Powered by Blogger.