Jina kamili; N'Golo Kante
Siku ya kuzaliwa; 29-March-1991
Miaka; 25
Mahali alipozaliwa; Paris, Ufaransa
Urefu; Meta 1.69 (Futi 5 na inchi 6½)
Nafasi; Kiungo mkabaji
Timu ya klabu; Chelsea
Jezi namba; 7
Timu ya taifa; Ufaransa
N'Golo Kante ambaye pia ana uraia wa Mali alianza maisha yake ya soka akiwa na miaka 8 katika klabu ya Js Suresnes ambapo alianza kuichezea mwaka 1999 mpaka mwaka 2010. Na baada ya hapo akaenda Boulogne mwaka 2010 mpaka 2011 na ndipo akapandishwa mpaka kikosi cha wakubwa ambapo alipandishwa mwaka 2011 na kufanikiwa kuichezea michezo 38 na kufunga magoli 3 kabla ya kuuzwa kwenda Caen mwaka 2013.
Caen ambayo aliichezea wakiwa ligi daraja la kwanza na kufanikiwa kuichezea mechi zake zote na mpaka kufanikiwa kupanda kuingia kwenye ligi kuu ya Ufaransa maarufu Ligue 1. Mpaka mwaka 2015 alipouzwa kwenda Leicester ambapo timu hiyo ya Caen aliichezea michezo 75 na kufunga magoli 4.
Usajili wake wa kwenda Leicester ulikamilishwa na skauti ambaye aliwai pia kusaidia usajili wa Vardy na Mahrez, Steve Walsh kwenda katika timu hiyo ya Leicester ambapo aliisaidia kubeba kombe la ligi kuu msimu huo huo.
Mwaka 2016 ndipo alisaini Chelsea kwa dau la £32 milioni (Paundi milioni 32) na kuichezea michezo michezo 27 mpaka sasa huku akiifungia goli moja alilofunga dhidi ya Man utd katika ushindi wa 4-0.
October, 23 alicheza dhidi ya Leicester kwa mara ya kwanza akiwa Chelsea na kuisaidia Chelsea kuikandamiza timu yake ya zamani kwa magoli 3-0 na yeye Kante kuchaguliwa kuwa mchezaji bora wa mchezo.
Usilolijua kuhusu Kante ingawa anaichezea Ufaransa lakini hajawai kuichezea timu yoyote ya vijana ya Ufaransa.
No comments:
Post a Comment