Wednesday, 30 August 2017

Ox aikataa Chelsea kisa nafasi

Baada ya Chelsea kukubaliana na Arsenal juu ya nyota Oxlade Chamberlain ambapo Arsenal ilikubali kupokea kiasi cha paundi milioni 40 ili kumuuza nyota huyo aungane na mabingwa wa UIngereza.

Chamberlain ameikataa ofa hiyo kwa kuwa anaona kama akitua Chelsea basi atacheza pembeni kama winga beki nafasi ambayo pia anaichezea Arsenal lakini yeye kama mchezaji anapendelea kucheza katikati. Kwa maana hiyo huenda akajiunga na Liverpool ambayo nayo inamtaka.

Chamberlain amekataa ofa ya kuendelea kubaki Arsenal na badala yake anatafuta timu ya kwenda kuichezea kabla dirisha la usajili kufungwa siku ya kesho usiku.

No comments:

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://www.facebook.com/photo.php?fbid=1405295759685033&set=t.100007345536843&type=3&theater} The moment you come is the moment we let you go away {facebook#https://www.facebook.com/jeshilangu}
Powered by Blogger.