Unamkumbuka yule nyota hatari wa Torino? Andrea Bellotti. Unakumbuka kama alishawai kutajwa kwa karibu kuja Chelsea? Sasa kuna habari mpya inamuhusu nyota huyo ambaye alikuwa anatazamiwa kuja Chelsea kuja kuziba pengo la Diego Costa kabla ya Chelsea kumpata Alvaro Morata.
Sasa nyota huyo anatakiwa kwa karibu na AS Monaco ambayo ipo tayari kuweka dau la euro milioni 80 ili kumchukua mshambuliaji huyo raia wa Italia. Bellotti licha ya kutakiwa na Chelsea alikuwa anatajwa pia kujiunga na vilabu kama Arsenal na AC Milan.
No comments:
Post a Comment