Mlinzi wa Chelsea ambaye ni raia wa Ufaransa, Kurt Zouma amekataa ofa ya kwenda kwa mkopo Valencia, ambayo ni klabu inayoshiriki Ligi Kuu Hispania maarufu kama La Liga.
Mlinzi huyo ambaye ameichezea Chelsea michezo 14 tu msimu uliopita amekuwa hana nafasi katika kikosi hicho na kwa yeye hategemei kuondoka klabuni hapo
"Nipo hapa na nitaendelea kubaki hapa, nataka kugombania nafasi katika nafasi yangu nikiwa hapa" amesema Kurt Zouma ambaye aling'aa sana msimu wa 2014-2015 kabla ya kupata majeraha yaliyomweka nje muda mrefu.
No comments:
Post a Comment