Tuesday, 11 July 2017

Salah ampongeza Rudiger

Mafahali wawili walioachana na klabu yao ya As Roma, Mohammed Salah na Antonio Rudiger waliojiunga katika klabu za Uingereza wote ni kama wanatamani kukutana tena.

Salah ambaye amejiunga na Liverpool alishawai kuichezea Chelsea ambayo imemsajili Rudiger, mchezaji mwenzake ambaye msimu uliopita walicheza wote As Roma na kuifanikisha kumaliza nafasi ya pili katika Ligi Kuu ya Italia maarufu kama Serie A.

Salah katika mtandao wa Instagram, ametuma picha akiwa na Rudiger pindi wakiwa As Roma na akaandika "Ni vyema kwa Chelsea (kwa kumsajili Rudiger) nategemea kukutana nae Inshaallah" akimaanisha anatamani sana kukutana na Rudiger akiwa kwenye klabu ya Chelsea wakati yeye akiwa Liverpool.

Lakini pia mchezaji wa zamani wa Chelsea, Didier Drogba amemkaribisha mchezaji huyo katika klabu ya Chelsea.

No comments:

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://www.facebook.com/photo.php?fbid=1405295759685033&set=t.100007345536843&type=3&theater} The moment you come is the moment we let you go away {facebook#https://www.facebook.com/jeshilangu}
Powered by Blogger.