Monday, 17 July 2017

Zidane akasirishwa na usajili wa Danilo

Kocha wa Real Madrid, Zinedine Zidane amekasirishwa na mchezaji wake Danilo ambaye anahitaji kuondoka klabuni hapo ili akatafute maisha sehemu nyengine.

Zidane ambaye kikubwa kilichomkasirisha kwa mchezaji huyo ni mtindo anaofanya wa kulazimisha kuuzwa ambapo Zidane anasema "Danilo ni msaliti"

Danilo amekuwa hana nafasi katika kikosi cha kwanza cha kocha huyo ambapo muda mwingi anashuhudia mwenzake, Carvajal akitumika.

Danilo anatakiwa kwa karibu na Chelsea ambapo kwa habari zilizopo ni kwamba Danilo ashakubaliana mahitaji binafsi na Chelsea kilichobaki ni kufanyiwa vipimo na Madrid kukabidhiwa wanachokidai.

Chelsea ipo tayari kutoa Paundi milioni 30 kwa mchezaji huyo.

No comments:

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://www.facebook.com/photo.php?fbid=1405295759685033&set=t.100007345536843&type=3&theater} The moment you come is the moment we let you go away {facebook#https://www.facebook.com/jeshilangu}
Powered by Blogger.