Mlinzi wa kulia aliyeichezea Benfica msimu uliopita, Nelson Semedo amejiunga rasmi na mabingwa wa Copa del Ley, Barcelona.
Semedo ambaye alikuwa akisakwa na baadhi ya vilabu vikubwa amekamilisha usajili huo huku akitazamiwa kuonyesha kiwango kikubwa kama cha mtangulizi wake, Dani Alves aliyeichezeaga klabu hiyo kwa mafanikio.
Kwa usajili huo inamaanisha Arsenal wamenusurika juu ya mlinzi wake wa kulia, Hector Bellerin aliyekuwa akihusishwa na wababe hao wa Hispania.
No comments:
Post a Comment