Chelsea imemruhusu kinda mwengine wa klabu hiyo kujiunga na klabu inayoshiriki Ligi daraja la kwanza maarufu Championships, Barnsley.
Kinda Ike Ugbo aliyekuwa anaichezea Chelsea-U23 aliichezea klabu hiyo kwa mafanikio ambapo msimu uliopita amefanikiwa kuifungia magoli 25 na sasa amejiunga na klabu hiyo kwa mkopo.
Kocha wa klabu hiyo Paul Heckingbottom amesema "Ugbo ni mchezaji mzuri, ana kasi na mrefu pia, ana kipaji na ni mchezaji bora" aliyasema maneno hayo wakati mchezaji huyo alipotangazwa rasmi kujiunga na klabu hiyo.
No comments:
Post a Comment