Kocha Antonio Conte mpaka sasa anahangaika kukijenga kikosi chake cha Chelsea ambapo bado kwake haijajulikana kama atasaini kuendelea kuwepo klabuni hapo.
Mwanzoni baada ya msimu kuisha ililipotiwa kuwa kocha huyo atasaini mkataba ndani ya klabu hiyo endapo tu Chelsea itawasajili wachezaji alioorodhesha kwamba anawataka.
Mwanzoni alikuwa na wazo la kuziba mapengo ya wachezaji ambao wameondoka klabuni hapo, ambapo alitaka kumtafuta mrithi wa Branislav Ivanovic ambaye alitimkia Zenit. Lakini pia alitaka kuziba pengo la John Terry, Cuadrado na wengine walioachana na klabu hiyo kipindi ambacho kocha huyo alipoiongoza klabu hiyo.
Lakini mpaka sasa ashafanikiwa kuwanasa Willy Caballero, Antonio Rudiger na Tiemoue Bakayoko lakini kocha huyo alimuhitaji Romelu Lukaku ambaye alimkosa.
Kumkosa mchezaji huyo ni kama kumemtibua kichwa na mpaka sasa anahangaika kutafuta mbadala hapo hapo pia mshambuliaji wake Diego Costa anaonekana kutokuendelea kuwepo klabuni hapo.
Sasa kinachosubiriwa mpaka sasa klabuni hapo je ni mshambuliaji gani atamfanya Conte apunguze munkari na awe tayari kuingia katika msimu mpya.
No comments:
Post a Comment