Saturday, 22 July 2017

Usajili umekamilika; Morata rasmi Chelsea

Alvaro Morata sasa ni rasmi ni mchezaji wa Chelsea. Baada ya fununu nyingi kuhusu mhispania huyo kutua Chelsea, sasa fununu hizo zimekuwa kweli baada ya jamaa huyo kutambulishwa rasmi leo mchana.

Morata amejiunga na Chelsea akitokea Real Madrid ambapo ameigharimu Chelsea kiasi cha Paundi milioni 70 zilizomfanya kuwa mchezaji ghali zaidi kununuliwa na mabingwa hao wa Uingereza lakini pia akimpiku mhispania mwenzake Fernando Torres kwa kuwa mhispania ghali zaidi. Torres alisajiliwa kwa kiasi cha Paundi milioni 50 na Chelsea akitokea Liverpool na kuweka rekodi hiyo ambayo leo Morata ameivunja.

No comments:

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://www.facebook.com/photo.php?fbid=1405295759685033&set=t.100007345536843&type=3&theater} The moment you come is the moment we let you go away {facebook#https://www.facebook.com/jeshilangu}
Powered by Blogger.