Baada ya kuwepo sintofahamu juu ya mshambuliaji Diego Costa aliyeipatia klabu hiyo mataji mawili ya ligi kuu katika misimu mitatu lakini sasa anataka kuachana na klabu hiyo na anataka kutimkia klabu yake iliyomtambulisha rasmi katika ulimwengu wa soka la kulipwa, Atletico Madrid.
Chelsea wametuma katika mtandao wa Instagram picha inayomuonyesha mshambuliaji mpya, Alvaro Morata akisaini mkataba wake wa miaka 5 kusalia klabuni hapo, picha ambayo ilipendwa pia na mchezaji muhispania mwenzake, Diego Costa hali ambayo wachambuzi wa mpira wametafsiri kwamba Diego Costa ameipenda picha hiyo kikubwa akimaanisha sasa anaona wa kurithi nafasi yake kashapatikana kwa hiyo yeye anakaribia kuondoka klabuni hapo.
No comments:
Post a Comment