Chelsea imefanya usajili mapema mwezi huu ambapo imemsajili kinda mwenye miaka 16, Ethan Ampadu.
Ethan Empadu alizaliwa tarehe 04-09-2000 akiwa ni mtoto wa mchezaji wa zamani maarufu kama Ampadu.
Mchezaji huyo amesajiliwa akitokea Exeter city aliyojiunga nayo akiwa na miaka 15 na ameichezea michezo kadhaa akiwa kama kiungo mkabaji.
Kwa upande wa timu ya taifa, Ethan ameichezea England-U16 na akaichezea Wales-U17 ambao ni uraia wa mama yake.
Mchezaji huyo anaitwa pacha wa David Luiz kutokana na mtindo wake wa nywele ukifanana na mlinzi huyo wa Chelsea. Ethan Ampadu ataitumikia Chelsea kwa ngazi ya akademi kabla ya kupandishwa timu ya wakubwa.
No comments:
Post a Comment