Klabu ya Arsenal ambao ni washika bunduki wa London imepeleka ofa klabuni Barcelona ili kumsaini nyota wa klabu hiyo, Rafinha.
Rafinha ambaye ameifungia Barcelona magoli 7 katika michezo 28 alioichezea klabu hiyo na Arsenal inamtazama kama mbadala baada ya kupoteza matumaini juu ya kumsajili kiungo wa AS Monaco, Lemar.
Arsenal imepoteza matumaini baada ya kuona AS Monaco wamekuwa wazito juu ya usajili wa Lemar na hii inaonekana kutokea baada ya klabu hiyo bingwa wa Ligue 1 kuwauza mapema wachezaji wake wawili ambao wote ni viungo, Bernardo Silva aliyesajiliwa na Man city, na Tiemoue Bakayoko aliyetimkia Chelsea.
No comments:
Post a Comment