Gazeti moja la Hispania limeripoti kwamba Pep Guardiola anatazamia kumuuza mshambuliaji wake Kun Aguero ambaye anaonekana hana nafasi katika kikosi cha Man city na Pep Guardiola anamtazama Gabriel Jesus kuwa chaguo lake la kwanza.
Mshambuliaji huyo ambaye amekuwa katika klabu hiyo kwa miaka 6 na aliisaidia kufunga goli lililoipatia Man city taji la Ligi Kuu Uingereza.
Kocha wa Chelsea, Antonio Conte amehangaika muda mrefu kutafuta saini ya mshambuliaji atakayemtumia msimu ujao na mpaka sasa kuna tetesi za kocha huyo akitajwa kuwawania Chicharito wa Bayer Leverkusen, Pierre Aubameyang wa Borussia Dortmund, Andrea Bellotti wa Torino na sasa Aguero nae anatajwa.
No comments:
Post a Comment