Sunday, 16 July 2017

Usajili umekamilika; Chelsea wampata rasmi Bakayoko

Kiungo wa Monaco, Tiemoue Bakayoko sasa amekuwa rasmi kiungo wa Chelsea baada ya mchezaji huyo kukamilisha usajili wa kuamia kwa mabingwa wa London ambapo usajili wake umeigharimu Chelsea kiasi cha Paundi milioni 40.
Na ujio wake atakabidhiwa namba 14.

Mchezaji huyo anakamilisha jumla ya wachezaji watatu waliosajiliwa na Conte msimu huu.

Antonio Rudiger nae wiki kadhaa alitambulishwa ndani ya Chelsea na kukabidhiwa 'jersey' namba 2 ambapo ilikuwa inavaliwa na Branislav Ivanovic aliyetimkia Zenit St.Petersburg.

Lakini pia klabu hiyo ikaziba pengo la Asmir Begovic aliyeuzwa kuelekea Bournemouth kwa dau la Paundi milioni 10 na Chelsea kuamua kumchukua kipa aliyeachwa na Man city, Willy Caballero.

No comments:

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://www.facebook.com/photo.php?fbid=1405295759685033&set=t.100007345536843&type=3&theater} The moment you come is the moment we let you go away {facebook#https://www.facebook.com/jeshilangu}
Powered by Blogger.