Mkongwe na gwiji wa Chelsea, Marcel Desailly ametoa mawazo yake juu ya wachezaji wawili wanaowaniwa na Chelsea ambao ni Emerick-Pierre Aubameyang wa Borussia Dortmund ambapo Chelsea inatajwa kupeleka ofa kwa mchezaji huyo kiasi cha Paundi milioni 65 na Alvaro Morata wa Real Madrid ambapo haijajulikana ni kiasi gani wababe wa London wameweka juu ya mchezaji huyo.
Desailly amesema kwake yeye anaamini Chelsea inamuhitaji sana Aubameyang kuliko inavyomuhitaji nyota wa kihispania, Alvaro Morata ambaye anaelezwa ameshajiunga na wenzake katika michezo ya kujipima nguvu kabla Ligi hazijaanza.
Chelsea ambayo imekamilisha baadhi ya sajili za wachezaji waliowataka kwa muda mrefu ambapo jumamosi ya leo imemtangaza rasmi Bakayoko kujiunga na klabu yao ina uhitaji wa mshambuliaji wa kati ambapo Diego Costa anaonekana hana chake tena ndani ya klabu hiyo, na mpaka sasa hajajiunga na wenzake katika mazoezi.
No comments:
Post a Comment