Friday, 14 July 2017

Usajili umekamilika; Chalobah asajiliwa na Watford

Kiungo wa Chelsea mwenye asili ya Sierra Leone anayeichezea timu ya taifa ya Uingereza, Nathaniel Chalobah amekamilisha usajili wake wa kujiunga na klabu ya Watford iliyomsajili kwa dau linalokadiriwa kuwa ni Paundi milioni 6.
Chelsea ilijaribu kufanya mazungumzo na mchezaji huyo ili asaini mkataba mpya ambao mkataba huo ulitarajia kushuhudia mchezaji huyo akipandishiwa mshahara mpaka kufikia Paundi 60,000 toka aliokuwa analipwa katika mkataba wake uliopita uliobakiza mwaka mmoja aliokuwa analipwa Paundi 5000.
Chalobah ameungana na kinda wenzake waliotokea kwenye akademi ya Chelsea kuondoka klabuni hapo. Ambao ni Solanke aliyeondokea Liverpool, Betrand Traore aliyetimkia Olympique Lyon, Ola Aina aliyejiunga na Hull city kwa mkopo na Loftus-cheek aliyejiunga na klabu ya Crystal Palace kwa mkopo wa muda mrefu.

No comments:

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://www.facebook.com/photo.php?fbid=1405295759685033&set=t.100007345536843&type=3&theater} The moment you come is the moment we let you go away {facebook#https://www.facebook.com/jeshilangu}
Powered by Blogger.