Friday, 14 July 2017

Makala; Makinda na ukuaji wao ndani ya Chelsea

Imetuuma wengi kwa huyu jamaa kuondoka Chelsea. Lakini mi napongeza kwa kile ambacho Chelsea inakifanya katika hili haswa kwa makinda waliozalishwa Cobham

Unaona kuna nafasi gani kwa mtu kama Chalobah kucheza wakati akina Bakayoko wanasajiliwa, alafu hapohapo unaskia taarifa kwamba Bakayoko sio wa mwisho kusajiliwa.....

Unadhani Traore ana nafasi gani ya kucheza wakati akina Bellotti na Morata wanapelekewa mpunga wakitakiwa kumwaga wino  darajani??? Alafu kumbuka Loic Remy nae karudi na kuna Batshuayi nae anataka namba....

Ola Aina anaanza vipi kucheza wakati Chelsea ishamleta Rudiger na bado inakesha kwa Alex Sandro.....

Sioni tatizo kwa wao kuuzwa lakini wakaja kusajiliwa baadae maana kwenye mikataba yao kuna vipengele vya kusajiliwa tena na Chelsea, waache wakakuze vipaji vyao....

Chalobah amesajiliwa na Watford na amesaini miaka 5.

#CFC1905

No comments:

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://www.facebook.com/photo.php?fbid=1405295759685033&set=t.100007345536843&type=3&theater} The moment you come is the moment we let you go away {facebook#https://www.facebook.com/jeshilangu}
Powered by Blogger.