Friday, 14 July 2017

Conte bado hajamaliza

Inasubiriwa muda ufike ili Bakayoko afanyiwe vipimo alafu atangazwe rasmi kujiunga na mabingwa wa Uingereza yaani Chelsea.

Mchezaji huyo ataigharimu Chelsea kiasi cha paundi milioni 40 ambazo Chelsea itahakikisha usajili huo unakamilika muda wowote siku ya Ijumaa ya tarehe 14 ya mwezi Julai.

Lakini ujio huo unaonesha nafasi finyu ya kiungo Nemanja Matic kuendelea na utawala wake katika kikosi cha Chelsea na kwa maana hiyo mchezaji huyo raia wa Serbia anashinikiza kuuzwa aweze akaanze maisha kwenye klabu nyengine. Ikumbukwe Man utd wanamfukuzia mchezaji huyu kwa karibu.

Lakini taarifa mpya zinasema ujio wa Bakayoko klabuni hapo haimaanishi utamfanya Conte aridhike na badala yake anatarajiwa kuongeza nyota mwengine katika nafasi ya kiungo.

No comments:

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://www.facebook.com/photo.php?fbid=1405295759685033&set=t.100007345536843&type=3&theater} The moment you come is the moment we let you go away {facebook#https://www.facebook.com/jeshilangu}
Powered by Blogger.