Nchi ya Tanzania siku ya jana ilipokea ugeni wa heshima wa klabu kongwe ya nchini Uingereza inayoshiriki Ligi Kuu Uingereza maarufu kama EPL, klabu ya Everton.
Klabu hiyo iliyotua nchini hapa ili kujiandaa na ligi kuu hiyo inayotarajiwa kuanza mwezi wa nane siku ya tarehe 12 ambapo ipo hapa ili kucheza na mabingwa wa kombe la Sportpesa, Gor Mahia ya nchini Kenya.
Klabu zote hizo zinazaminiwa na kampuni hiyo ya kuchezesha michezo ya bahati nasibu ambapo makao yake ni nchini Kenya.
Klabu ya Everton imepanga kucheza mchezo wa kirafiki na klabu hiyo ambapo imetua nchini na wachezaji wake wote ambao huwa wapo kwenye kikosi cha kwanza cha timu hiyo.
Mchezo huo utachezwa mida ya saa 11 jioni katika uwanja wa Taifa unaopatikana jijini Dar es Salaam, ambapo dunia na wapenda soka watapenda kujua nini kitaenda kutokea katika mchezo huo.
Kikosi cha Everton kilichotua ni;
Maarten Stekelenburg, Mateusz Hewelt, Chris Renshaw, Tom Davies, Phil Jagielka, Ashley Williams, Callum Connolly, Jonjoe Kenny, Michael Keane, Muhamed Besic, Leighton Baines, Morgan Schneiderlin, James McCarthy, Davy Klaassen, Gareth Barry, IdrissaGanaGueye, Joe Williams, Kieran Dowell, Kevin Mirallas, Wayne Rooney, Aaron Lennon, Dominic Calvert-Lewin, Ademola Lookman, Matthew Pennington, Yannick Bolasie.
No comments:
Post a Comment