Mshambuliaji wa Arsenal, Lucas Perez huenda akaungana na klabu ya Uturuki, Fenerbahce ambayo ipo kwenye mazungumzo na Arsenal ili kumchukua mshambuliaji huyo kwa mkopo.
Fenerbahce imeonyesha nia ya kumtaka mshambuliaji huyo na imeshaanza mazungumzo na kon ili klabu hiyo ya London ili kumchukua mhispania huyo ambaye alisajiliwa na Arsenal katika dirisha kubwa lililopita.
Perez mwenye miaka 28 anatabiriwa kuondoka klabuni hapo kwa maana kwa kuwepo michuano ya Kombe la Dunia mwaka ujao basi inaonekana atataka kupata timu itakayompa nafasi ya kucheza zaidi ambapo hapoArsenal inaonekana ana nafasi finyu ya kuwa kikosi cha kwanza ukizingatia Arsenal imemsajili mshambuliaji mwengine, Lacazzete.
No comments:
Post a Comment