Winga wa Chelsea, Pedro kurudi London baada ya uchunguzi wa kwanza kufanyika.
Kiungo huyo raia wa Hispania jana katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Arsenal alipata ajali iliyomfanya kushindwa kuendelea kucheza na kufanyiwa mabadiliko katika dakika hiyo ya 29 na kukimbizwa hospitalini. Baada ya uchunguzi wa kitabibu kufanyika imeonekana itakuwa vyema kwa mchezaji huyo kurudi Uingereza ili kwenda kuangaliwa zaidi.
Jana usiku kabla ya taarifa hiyo kuhusu kutakiwa kurudi kwake Uingereza kulikuwa na uonekano kwamba anaweza kupona haraka na kuungana tena na timu ambayo ipo barani Asia kwa ajili ya kujiandaa na msimu mpya, lakini sasa inaonekana uwezekano huo haupo na mchezaji huyo atarudi London akiisubiri timu imalize ziara yake barani huko.
No comments:
Post a Comment