Sunday, 23 July 2017

Pedro anaendelea vizuri

Baada ya kupata majeraha katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Arsenal, nyota na winga machachari wa Chelsea, Pedro hatimae amewatoa hofu mashabiki waliokuwa na wasiwasi kuhusu hali yake.

Katika mtandao wa Twitter,mhispania huyo alipiga picha akiwa kitandani hospitalini akifuata na maneno yaliyosomeka "Ni tukio la kushangaza, Lakini naendelea salama".

Ilikuwa katika dakika ya 29 ambapo ilipigwa pasi ndefu golini kwa Arsenal na ndipo winga huyo akawa anaukimbilia na ndipo akagongana na kipa wa Arsenal, David Ospina ambaye nae alikuwa katika harakati za kuokoa shambulizi hilo. Na ndipo kipa huo akampiga kwa bahati mbaya kichwani na Pedro akadondoka.

Na kwa hali inavyoonesha mchezaji huyo hajapata majeraha makubwa kwa maana hiyo huenda nyota huyo  akaruhusiwa kutoka muda wowote.

No comments:

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://www.facebook.com/photo.php?fbid=1405295759685033&set=t.100007345536843&type=3&theater} The moment you come is the moment we let you go away {facebook#https://www.facebook.com/jeshilangu}
Powered by Blogger.