Mshambuliaji ghali zaidi kwenye kikosi cha Chelsea, Alvaro Morata anatazamiwa kuungana na Chelsea muda wowote kuanzia sasa hivi mara baada ya kutuma picha katika mtandao wa Instagram yenye maneno yanayoelezea kuungana kwake na klabu yake mpya.
Na huenda mchezaji huyo akawa kwenye kikosi kitakachocheza mchezo wa kirafiki na Bayern Munich siku ya tarehe 25.
Morata ambaye amesajiliwa Chelsea akitokea Real Madrid kwa dau lililomfanya kuwa mhisphaania ghali zaidi kuwai kununuliwa kwa dau la Paundi milioni 70 anatazamiwa kuchukua nafasi ya mhuspania mwenzake, Diego Costa anayeonekana kutokuendelea kuwepo katika mipango ya kocha Antonio Conte.
Lakini pia mshambuliaji huyo ambaye aliwai kufanya kazi chini ya Antonio Conte aliushuhudia mchezo wa kirafiki baina ya klabu yake hiyo mpya ilipomenyana na Arsenal na kupitia mtandao wa Instagram alituma picha ya mchezo huo huku akionyeshwa kufurahishwa kwa matokeo hayo.
|
Alvaro Morata akiwa uwanja wa ndege akienda kuungana na Chelsea barani Asia |
No comments:
Post a Comment