Saturday, 22 July 2017

Conte amsifia Batshuayi

Baada ya mchezo wa leo baina ya watani wa jiji moja yaani Chelsea dhidi ya Arsenal nchini China ambapo Chelsea imeshinda magoli 3-0.

Kocha wa Chelsea ametoa takwimu zake kuhusiana na mchezaji Michy Batshuayi ambaye katika mchezo huo alifanikiwa kufunga mara 2 na kutoa pasi ya bao lililofungwa na Willian.

"amekuwa na kiwango bora nani vizuri kumtazama. Anahitaji kukua kwenye soka lake na sisi kama makocha tupo ili kumfanya awe na kiwango bora" alisema Antonio Conte juu ya mchezaji huyo aliyesajiliwa msimu uliopita akitokea Olympique Marseille.

Batshuayi amekuwa na kiwango bora katika michezo ambayo Chelsea imecheza kujiandaa na msimu mpya ambapo katika mchezo wa awali katika kiwanja cha mazoezi cha Cobham ambapo ilicheza dhidi ya Fulham na Batshuayi au kwa jina la utani Batman akaiongoza vyema klabu yake kupata ushindi wa mabao 8-2 ambapo alifunga mara 2.

No comments:

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://www.facebook.com/photo.php?fbid=1405295759685033&set=t.100007345536843&type=3&theater} The moment you come is the moment we let you go away {facebook#https://www.facebook.com/jeshilangu}
Powered by Blogger.