Wednesday, 5 July 2017

Ni kama Sandro ameiroga Chelsea

Beki wa Juventus, Alex Sandro anaonekana kuivutia Chelsea kwa karibu zaidi mpaka kuifanya Chelsea ichanganyikiwe juu ya mchezaji huyo.
Ujue imekuaje? Baada ya ofa ya £60milioni ambayo Chelsea iliipeleka Juventus ili kuweza kumsajili mlinzi huyo ingawa ofa hiyo ni kama haijashawishi kuwalewesha vigogo wa Juventus, na sasa Chelsea imeandaa mbinu mpya katika kumuwania mchezaji huyo.
Unajua mbinu gani?
Chelsea wameamua kuishawishi Juventus kwa kuwaambia watawapa fedha na Marcos Alonso ili waruhusu Sandro atue darajani.
Marcos Alonso ambae ametua klabuni hapo kabla ya msimu uliopita kuanza ambapo alisajiliwa akitokea Fiorentina inaonekana ndo atatumika kama chambo kwa Juventus ambao na wao watashikishwa na pesa kidogo ili imuuze Alex Sandro.

No comments:

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://www.facebook.com/photo.php?fbid=1405295759685033&set=t.100007345536843&type=3&theater} The moment you come is the moment we let you go away {facebook#https://www.facebook.com/jeshilangu}
Powered by Blogger.