Mpaka sasa taarifa zilizopo kutoka kwenye gazeti moja la Hispania zinaeleza kwamba mshambuliaji mahiri wa taifa hilo anayekipiga Chelsea, Diego Costa anakaribia kusaini muda wowote kuanzia sasa katika klabu yake ya zamani ya Atletico Madrid.
Mshambuliaji huyo atasajiliwa na klabu hiyo ambayo imepewa adhabu ya kutokusajili mpaka kufikia mwezi januari mwaka 2018 lakini klabu hiyo imesema itakuwa tayari kumsajili mchezaji huyo ingawa hatocheza mchezo wowote katika klabu hiyo badala yake atakuwa akifanya nayo tu mazoezi mpaka adhabu yao iishe.
No comments:
Post a Comment