Friday, 7 July 2017

Morata sasa aitaka Chelsea

Mshambuliaji wa Real Madrid, Alvaro Morata sasa aitaka Chelsea. Ndiyo anaitaka Chelsea baada ya dili lake lililokuwa linakaribia kukamilika la kwenda Man utd kuharibika.

Limeharibikaje?
Baada ya klabu ya Man utd kupeleka ofa ya kumtaka mshambuliaji huyo walifanya makubaliano na mchezaji huyo na wakakubaliana. Lakini kikwazo kikaja kwa klabu yake hiyo inayonolewa na Zinedine Zidane ambapo ilitaka dau kubwa ambalo Man utd wameshindwa kulimudu na kuamua kuachana nae.

Sasa aitaka tena Chelsea
Baada ya ofa hiyo kuharibika sasa Alvaro Morata ameona itakuwa ni bora akarudiana na Chelsea klabu inayonolewa na Antonio Conte, kocha ambaye waliwai kufanya kazi pamoja wakiwa Juventus.
Morata hana uhakika wa nafasi katika kikosi cha Zidane na anachokitaka msimu wa 2017-2018 umkute akiwa klabu tofauti na klabu yake ya sasa. Na dau lake linatajwa kuwa si chini ya £75milioni.

No comments:

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://www.facebook.com/photo.php?fbid=1405295759685033&set=t.100007345536843&type=3&theater} The moment you come is the moment we let you go away {facebook#https://www.facebook.com/jeshilangu}
Powered by Blogger.