Nyota wa Everton, Kevin Mirallas amempiga dongo nyota wa zamani wa klabu hiyo ambaye kwa sasa ametimkia Manchester united, Romelu Lukaku.
Nyota huyo alipokuwa kwenye mahojiano alisema "kila mtu anautambua mchango wa Lukaku kwa Everton, amefunga magoli mengi ndani ya Everton lakini bado naona Everton ni sehemu sahihi kuliko Man utd"
Romelu Lukaku ambaye ameichezea Everton jumla ya michezo 133 na kuifungia magoli 71 kwa kwa misimu minne amehamia Man utd ambayo mpaka sasa ameshaichezea michezo 3 na kufunga mara mbili katika michezo ya kujiandaa na msimu mpya, huku akisajiliwa na klabu kwa dau la Paundi milioni 75.
"Naamini kwa wachezaji waliosajiliwa wataziba pengo la Lukaku na watakuwa bora zaidi yake" a Mirallas akiwaelezea washambuliaji wapya waliosajiliwa na klabu hiyo ambao ni Rooney ambaye mpaka sasa ameshaifungia klabu yake hiyo mpya jumla ya magoli 2 katika michezo 2, na wengine ni Sandro na Klaasen aliyetokea klabu ya Ajax
.
No comments:
Post a Comment