Saturday, 22 July 2017

Matic kutumika kulipa kisasi kwa Lukaku

Chelsea imepanga kumtumia kiungo wake Nemanja Matic anayehusishwa kujiunga na matajiri wa jiji la Manchester, Manchester united.

Manchester united iliyo chini ya kocha mreno aliyewai kuifundisha Chelsea, Jose Mourinho ilikuwa inahitaji saini ya mserbia huyo a anaonekana kupoteza nafasi katika kikosi cha kwanza mara baada ya Chelsea kumsajili kiungo Tiemoue Bakayoko.

Na kwa maana hiyo tajiri wa Chelsea, Roman Abramovich anataka kutumia usajili huo ili kuiadhibu klabu hiyo ya Mashetani wekundu mara baada ya mashetani hao kumsajili mshambuliaji Romelu Lukaku aliyekuwa karibu kujiunga na Chelsea.

Mourinho ambaye mpaka sasa ameshakamilisha sajili za wachezaji wawili Romelu Lukaku aliyemsajili akitokea Everton kwa dau la Paundi milioni 75 na mlinzi wa zamani wa mabingwa wa Ureno, Victor Lindelof anamtazamia kiungo Nemanja Matic aweze kuungana nae tena ili kuwa na kikosi kipana kabla ya kuanza kwa msimu mpya.

Thamani ya Mserbia, Nemanja Matic mwenye miaka 28 inatajwa kufikia Paundi milioni 50.

No comments:

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://www.facebook.com/photo.php?fbid=1405295759685033&set=t.100007345536843&type=3&theater} The moment you come is the moment we let you go away {facebook#https://www.facebook.com/jeshilangu}
Powered by Blogger.