Mlinda mlango wa Bournemouth ambaye msimu uliopita alikuwa Chelsea, Asmir Begovic amempiga kocha wa Chelsea, Antonio Conte ambaye alikuwa chini yake kwa msimu huo ambapo kocha huyo aliisaidia Chelsea kubeba taji la ligi kuu Uingereza.
"Kiukweli nimecheza chini ya makocha bora lakini nachoona Jose Mourinho ni kocha bora zaidi" alisema Asmir Begovic ambaye ameuzwa kwenda Bournemouth kwa dau la Paundi milioni 10.
Jose Mourinho ambaye aliifundisha Chelsea kabla ya Conte ndie aliyemnunua kipa huyo na kipa huyo akacheza jumla ya michezo 19 akiwa chini ya Mourinho wakati chini ya Conte amecheza michezo 8 tu.
"Ana mawasiliano mazuri kwa wachezaji na mazoezini ni mtu poa sana" alisema kipa huyo raia wa Bosnia akielezea sifa za Mourinho "Najivunia sana kuwa chini yake (Mourinho)"
No comments:
Post a Comment