Monday, 17 July 2017

Mapya yaibuka kwa Chicharito

Juu ya nia ya Conte kumsajili mshambuliaji atakayechukua nafasi ya Diego Costa kulikuwa na wazo la kumsajili mshambuliaji wa zamani wa Man utd ambaye kwa sasa anaichezea Bayer Leverkusen.

Yadhihirika kumbe klabu iliyokuwa inapambana na Chelsea katika kuwania saini ya mchezaji huyo, West Ham ndio wanaokaribia au kuonekana watamsajili mshambuliaji huyo ambaye ni mfungaji bora wa muda wote wa nchini kwake Mexico.

Javier Hernandez au Chicharito anaonekana kuungana na West Ham na sio Chelsea kwa vile tu Slaven Bilic ambaye ni kocha wa West Ham amemfanya mshambuliaji huyo kuwa chaguo la kwanza na sio Chelsea ambayo inatazama washambuliaji wengi.

No comments:

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://www.facebook.com/photo.php?fbid=1405295759685033&set=t.100007345536843&type=3&theater} The moment you come is the moment we let you go away {facebook#https://www.facebook.com/jeshilangu}
Powered by Blogger.