Baada ya kutajwa kwa muda mrefu juu ya usajili wa mbrazili, Danilo kutua kwake Chelsea. Sasa habari hizo zimenogeshwa na gazeti moja la kibrazili.
Chelsea kukaribia kumnasa Danilo. Ndio gazeti hilo lilivyoeleza likiendelea kwa kuandika kwamba Chelsea ndio inaongoza katika harakati za kumsajili mchezaji huyo akitokea Real Madrid.
Danilo mwenye miaka 26 inataarifiwa ashakubaliana na mabingwa hao wa Ligi kuu Uingereza mahitaji binafsi na sasa bado Madrid na Chelsea tu kukamilisha usajili huo.
Lakini pia inataarifiwa kwamba muda wowote huenda Danilo akakwea pepa kufika London ambapo akafanyiwa vipimo na klabu hiyo ambayo inadaiwa kutoa kiasi cha Paundi milioni 30 kumsajili mlinzi huyo.
No comments:
Post a Comment