Monday, 17 July 2017

Mapacha wa Chelsea na ubora wao

Kiungo mpya Tiemoue Bakayoko ambaye ametua Chelsea akitokea AS Monaco kwa dau la Paundi milioni 40 ametoa neno juu ya kucheza kwake sambamba na mfaransa mwenzake, N'golo Kante.
"Kwanza ni jambo jema sana kuwepo Chelsea na ni nafasi nzuri kucheza sambamba na mchezaji bora kama Kante, amekuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu msimu wa 2016-2017 na kwa maana hiyo nitafanya vizuri sana nikicheza pamoja nae" alisema Bakayoko akimwongelea 'pacha' wake N'golo Kante.
"Naamini itakuwa nafasi nzuri kwangu kufanya vizuri kwa maana nipo karibu na mchezaji bora. Nimewai kucheza nae pamoja tukiwa timu ya taifa (Ufaransa) nadhani kwa hivyo tunajuana mi nayeye"
Bakayoko anatazamwa kuingia kwenye kikosi cha kwanza mara baada ya Matic kuonekana hatoendelea kuwepo klabuni hapo na anatajwa kujiunga na Inter Milan au Man utd zinazomwania kwa karibu.

No comments:

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://www.facebook.com/photo.php?fbid=1405295759685033&set=t.100007345536843&type=3&theater} The moment you come is the moment we let you go away {facebook#https://www.facebook.com/jeshilangu}
Powered by Blogger.