Mshambuliaji, Loic Remy ambaye sasa amerudi Chelsea akitokea Crystal Palace alipokuwa kwa mkopo huenda akang'atuka Chelsea.
Hii inatazamika kutokea endapo Chelsea itasajili mshambuliaji mwengine, ambapo tayari ashapokea ofa za kutakiwa na Everton na Olympique Marseille.
Remy atasafiri pamoja na Chelsea kwenda China ambapo Chelsea itacheza michezo ya kirafiki ambapo tarehe 22 mwezi huu itacheza na Arsenal, tarehe 25 itakutana na Bayern Munich kabla ya kumaliza na Inter Milan tarehe 28 mwezi huu huu.
No comments:
Post a Comment