Thursday, 13 July 2017

Man utd; Mmoja kati ya hawa lazima avae Chevrolet

Mmoja wao kati ya Matic wa Chelsea, Eric Dier wa Tottenham au Radja Nainggolan wa AS Roma anaweza kujiunga na klabu hiyo.

Eric Dier anadaiwa kudai anataka kuondoka klabuni hapo na analazimisha dili la kuhamia Man utd likamilike haraka. Nae Nemanja Matic ambaye anaona nafasi yake ya kubaki Chelsea katika kikosi cha kwanza baada ya klabu hiyo kukaribia kumsajili Bakayoko nae anataka kuondoka na mpaka sasa anafanya mazoezi peke yake.

Lakini pia Nainggolan nae anatajwa kutua Man utd ambapo ataungana na mastaa wenzake wa As Roma walioachana na klabu hiyo na kuamia EPL ambao ni Salah aliyejiunga na Liverpool na Antonio Rudiger aliyetua Darajani.

No comments:

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://www.facebook.com/photo.php?fbid=1405295759685033&set=t.100007345536843&type=3&theater} The moment you come is the moment we let you go away {facebook#https://www.facebook.com/jeshilangu}
Powered by Blogger.