Kipa namba moja wa Hispania anayeichezea Man utd, Davi De GEa amepeleka maombi kwa matajiri hao wa Manchester ya kutaka kuondoka klabuni hapo na yeye inasemekana anataka kuungana na klabu ya Real Madrid ambao na wao walionyesha nia kubwa ya kumtaka kipa huyo ambaye msimu uliopita ameingia kwenye kikosi bora cha Ligi Kuu UIngereza.
David De Gea amabyae ilibaki kidogo aungane na mabingwa hao wa kihistoria wa klabu bingwa ya Ulaya, Real Madrid lakini kukatokea kikwazo ikashindikana kuondoka lakini sasa kipa huyo inadaiwa kaanza kulazimisha dili hilo likamilike ili aachane na klabu hiyo.
No comments:
Post a Comment