Baada ya kocha wa Man city, Pep Guardiola kuamini kwamba ashamnyakua mlinzi wa Juventus, Dani Alves baada ya kukubaliana mahitaji ya mwanzo sasa ni kama dili linakaribia kuharibika.
Inasemekana Alves alishakubaliana na Man city na ikaaminika muda wowote atamwaga wino katika klabu hiyo lakini sasa hali ni tete baada ya matajiri wa Paris, PSG kumpa dau kubwa mchezaji huyo ambapo wameandaa mshahara wa Paundi 230,000 kwa wiki. Mshahara unaoonekana utamtamanisha Alves na kuungana na klabu hiyo.
No comments:
Post a Comment