Rais wa klabu ya Torino ya Italia, Urbano Cairo amesema yupo tayari kumuuza mchezaji anayewaniwa na Chelsea, Andrea Bellotti.
Mshambuliaji huyo ambaye alikuwa mfungaji bora wa timu yake hiyo akiwatoa udenda klabu kubwa za Ulaya juu ya kiwango chake ameelezewa thamani yake na tajiri huyo.
"Mpaka sasa hakuna timu iliyoleta ofa ya kumsajili Bellotti, ingawa kama ikitokea basi itatakiwa ilipe kiasi cha Euro milioni 100 (ambacho ni sawa na Paundi milioni 89)" alisema tajiri huyo.
Bellotti ana miaka 23.
No comments:
Post a Comment