Baada ya kumkosa Romelu Lukaku aliyetimkia Man utd, sasa Chelsea wamefika mpaka Borussia Dortmund na kumtaka mshambuliaji wa klabu hiyo ambaye ni raia wa Gabon, Pierre Aubameyang ambaye magoli yake 31 katika klabu hiyo yamemfanya kuwa mfungaji bora wa ligi kuu Ujerumani maarufu kama Bundesliga msimu wa 2016-2017.
Chelsea yenyewe imesema ipo tayari kutoa Paundi milioni 70 ili kumsajili mchezaji huyo anayewaniwa pia na AC Milan klabu ambayo aliitumikia mwanzo japo alikuwa akitolewa kwa mkopo.
Sio Chelsea na AC Milan tu bali hata matajiri wa jiji la Paris, PSG na wao wameonyesha nia ya kumtaka mshambuliaji huyo.
No comments:
Post a Comment