Saturday, 22 July 2017

Mambo unayopaswa kuyajua kwa Stamford Bridge mpya

Chelsea imepanga kuufanyia marekebisho uwanja wake wa Stamford Bridge katika mwendelezo wake wa kuifanya klabu na uwanja huo kuzidi kuwa kubwa na wenye historia kubwa kati ya klabu bora Ulaya na Uingereza pia. Kuna vitu unatakiwa kuvijua katika mwendelezo huu wa ujenzi na upanuzi mkubwa wa uwanja huu.
Historia ya Stamford Bridge
Stamford Bridge ulianza kutumika rasmi mwaka 1877 ambapo mwanzoni ulikuwa unatumika na klabu ya London Athletic Club kabla ya Gus Mears kuianzisha Chelsea ambayo ilianza kuutumia uwanja huo mnamo mwaka 1905 kabla ya mmliki huyo kufariki mwaka 1912.

Chelsea itatumia uwanja gani wakati Stamford ukiwa kwenye matengenezo?
Toka mwaka huo 1905 mpaka leo Chelsea imekuwa ikiutumia uwanja wa Stamford Bridge unaopatikana kwenye mtaa wa Fulham magharibi mwa jiji la London, na baada ya uwanja huo kuingia kwenye matengenezo basi hautotakiwa kutumika kwa maana hiyo klabu hiyo itapaswa kufanyia shughuli zake sehemu nyengine.

Je ni uwanja gani?
Uwanja gani klabu hiyo utatumia katika michezo yake, ni swali ambalo bado halijapata jibu mpaka sasa maana ilitegemewa uwanja wa Wembley ndo utatumika lakini uwanja huo kumekuwa na makatazo toka kwa wananchi wanaoishi pembezoni mwa uwanja huo wakidai kutumika kwa uwanja huo na Chelsea kutaongeza foleni na baadhi ya tabia hatarishi kutokana na msongamano wa watu wengi watakaokuwa wanaongozana katika michezo ya klabu hiyo.

Ni lini Stamford itaanza kurekebishwa?
Msimu wa 2017-2018 ndo msimu unaotajwa kuwa msimu wa Chelsea kuutumia uwanja huo ambapo unatarajiwa kujengwa mpaka msimu wa 2021-2022 ambapo ndo unatarajiwa kukamilika.

Kwa kiasi gani utaongezeka?
Kwa sasa Stamford Bridge unaweza kuingiza jumla ya mashabiki 41,000 na baada ya marekebisho unatarajiwa kufikia jumla ya mashabiki 60,000.

Serikali inasemaje?
Meya wa jiji la London, ndugu Sadiq Khan amesema "nafurahishwa na jitihada hizi za kupanuliwa kwa kiwanja hiki na naona London ikiendelea kukua kimichezo na kuwa kitovu kikubwa cha mafanikio katika michezo"
Uwanja huo utaigharimu Chelsea kiasi cha Paundi milioni 500.
Uwanja wa Stamford Bridge utakavyokuwa baada ya matengenezo msimu wa 2021-2022

No comments:

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://www.facebook.com/photo.php?fbid=1405295759685033&set=t.100007345536843&type=3&theater} The moment you come is the moment we let you go away {facebook#https://www.facebook.com/jeshilangu}
Powered by Blogger.