Saturday, 22 July 2017

Chelsea na Arsenal mbele ya akina Jet Li

Klabu wababe wa jiji la London, Arsenal na Chelsea zinategemewa kumenyana siku ya leo ya tarehe 22-Julai huko katika jiji la kifahari nchin China, Beijing.

Klabu hizo zitamenyana katika mchezo huo katika kujiandaa na msimu mpya wa 2017-2018 ambapo kwa upande wa Chelsea huu ni mchezo wa pili wa kirafiki kucheza mara baada ya siku kadhaa nyuma kumenyana na jirani yake, Fulham na Chelsea kushinda 8 kwa 2. Lakini Arsenal wataingia katika mchezo huu wakiwa tayari washacheza michezo kadhaa nyuma ambapo wamecheza michezo kadhaa nchini Australia kabla ya sasa kutua nchini China.

Beijing National Stadium ndio uwanja utakaotumika katika mchezo huo ambapo uwanja huo una uwezo wa kuingiza mashabiki 91,000 na ulifunguliwa mwaka 2008.

Chelsea wataingia katika mchezo huu huku ikiwakosa nyota wake Eden Hazard aliyepata majeraha katika majukumu ya timu ya taifa na kiungo mpya wa klabu hiyo, Tiemoue Bakayoko nae hatokuwepo.

No comments:

Post a Comment

Johnny MaLcom x

{picture#https://www.facebook.com/photo.php?fbid=1405295759685033&set=t.100007345536843&type=3&theater} The moment you come is the moment we let you go away {facebook#https://www.facebook.com/jeshilangu}
Powered by Blogger.