Inasubiriwa Ijumaa ikamilike kukucha taarifa za Chelsea kusajili mchezaji mwengine kwa bei mbaya itangazwe baada ya siku kadhaa Chelsea kufanya biashara na As Roma sasa anayesubiriwa ni kijana wa miaka 26, Tiemoue Bakayoko.
Na kiungo huyo anaonekana kuchochea usajili huo mara baada ya kuonekana na viashiria vingi vya kuungana na mabingwa hao.
Jana mapema kaka yake na mchezaji huyo ambaye pia ni wakala wake alituma katika mtandao wa Snapchat kiashiria kinachoiwakilisha Chelsea hali ambayo inatafsiriwa anaonekana anachochea dili la mdogo wake kutua Chelsea.
Lakini sasa tena mwenye Bakayoko katika mtandao wa Instagram ametuma picha akiwa na kijana aliyevalia fulana au 'jersey' ya Chelsea ambapo wachambuzi wa soka wanatafsiri kwamba kwa asilimia kubwa anaweza akavaa uzi wa Chelsea msimu ujao.
No comments:
Post a Comment