Kitendawili mpaka sasa hakijaeleweka nani wa kukitegua, labda viongozi wa Chelsea na wa Torino au wa Chelsea na wa Borussia Dortmund ndio ambao wanaweza kutoa urahisi wa kukitegua kitendawili hiko.
Kitendawili hiko ni kinasema, je ni nani atakuwa mshambuliaji mpya wa Chelsea msimu ujao?
Ndio ni kitendawili kigumu sana kwa kila mpenda soka mara baada ya yule aliyekuwa anacheza nafasi hiyo katika klabu hiyo ya London Magharibi, Diego Costa kuonekana haitajiki tena Darajani.
Na wanaotazamiwa kuchukua nafasi hiyo wakipewa uzito watu wawili, mmoja ni mchezaji wa Italia anayeichezea klabu ya Torino na mwengine ni raia wa Gabon, Emerick Aubameyang.
Kila siku mapya yanazidi kutokea lakini jipya safari hii ni mara baada ya klabu ya Torino kutambulisha jezi zitakazotumiwa msimu ujao na klabu hiyo bila uwepo wa nyota wao huyo Andrea Bellotti.
Ambapo hiyo imetafsiriwa kwamba huenda klabu hiyo haitazami kuendelea kuwa nae mshambuliaji wao bora wa msimu uliopita. Ambapo hiyo inatafsiriwa kwamba klabu zinazomwania mchezaji huyo ni kama zimechochewa katika jitihada zao za kufanya usajili haraka.
Je ni Bellotti au Aubameyang kuvaa viatu vya Diego Costa?
No comments:
Post a Comment